Maukibu ya watu wa Karbala inaomboleza kifo cha Kiongozi wa waumini (a.s).

Watu wa Karbala wamefanya matembezi ya pamoja katika mji mtukufu wa Najafu kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).

Matembezi yamefanywa kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Watu wa Karbala wameomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib ndani ya haram yake takatifu.

Kufanya maukibu ya kuomboleza kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ni utamaduni wa watu wa Karbala katika matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s).

Maukibu ya pamoja inaundwa na maukibu za Karbala, vikundi vya Husseiniyya na wakazi wa mji wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: