Ili kuboresha huduma kwa mazuwaru.. Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amekutana na katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aaludhiyaau-Dini amekutana na katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya Sayyid Issa Khurasani, na kujadili njia za kuboresha huduma kwa mazuwaru.

Kikao hicho kimefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya, na kuhudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, ambao ni Sayyid Liith Mussawi, Sayyid Jawadi Hasanawi, Sayyid Mhandisi Muhammad Ashqar, mkuu wa ofisi ya katibu mkuu wa Ataba na rais wa kitengo cha uhusiano Muhammad Ali Azhar.

Mwishoni mwa kikao, Mheshimiwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu amampa zawadi katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya Sayyid Issa Khurasani na ujumbe aliofuatana nao, kutokana na kazi kubwa wanayofanya ya kuhudumia mazuwaru wa Imamu Ali (a.s) katika mji wa Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: