Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake imepata nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya Qur’ani.

Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imepata nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya Qur’ani yaliyoandaliwa na idara ya malezi ya Iraq, jumla ya wanafunzi wake 21 wamefuzu kwenye mashindano hayo.

Kiongozi wa Maahadi Ustadhat Manaar Aljaburi amesema “Wanafunzi (21) kutoka kwenye Maahadi zetu hapa Iraq wamevuna juhudi zao za kusoma na kuhifadhi Qur’ani tukufu, wamepata nafasi za kwanza kwenye mashindano ya Qur’ani yaliyoandaliwa na idara ya malezi ya Iraq”.

Akaongeza kuwa “Maahadi hutoa uangalizi maalum kwa wanafunzi wanaosoma Qur’ani pamoja na kugawa zawadi mbalimbali”
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: