Majmaa-Ilmi imehudhuria shughuli ya kubadilisha bendera ya Muslim bun Aqiil (a.s).

Ujumbe kutoka Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, umehudhuria shughuli ya kubadilisha bendera ya Muslim bun Aqiil (a.s) katika mji wa Najafu.

Majmaa imewakilishwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu.

Shughuli ya kubadilisha bendera ya balozi wa Imamu Hussein (a.s) ni kielelezo cha kuomboleza kifo chake na kuanza kwa msimu wa huzuni za tukio hilo.

Kumbuka kuwa Majmaa-Ilmi huhudhuria kila mwaka katika maombolezo ya shahidi wa kwanza miongoni mwa mashahidi wa Twafu Muslim bun Aqiil (a.s), ambaye vizazi na vizazi vinasoma kutoka kwake uaminifu, ushujaa na msimamo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: