Sayyid Swafi aongea na watumishi wa kitengo cha uboreshaji: Pambeni beji lenu la mafunzo kwa dua ya Makaarimul-Akhlaaq.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amekutana na watumishi wa idara ya uboreshaji na maendeleo endelevu akawataka wanufaike na dua ya Makaarimul-Akhlaqi ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s).

Ameyasema hayo baada ya kumpokea rais wa kitengo hicho Dokta Muhammad Hassan Jaabir, mbele ya katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na mjumbe wa kamati kuu Dokta Abbasi Dida Mussawi na Huquqi Kadhim Ibada.

Sayyid Swafi amehimiza umuhimu wa kuchota elimu katika dua ya Makaarimul-Akhlaq na msingi wa masomo ya kimaadili, hakika dua hiyo inamafundisho muhimu ya kibinaadamu.

Akaongeza kuwa “Ratiba hiyo inaweza kuwa pana ikajumuisha mambo mengi ya kimalezi na kijamii, hivyo inatakiwa kuwa na selebasi ya masomo inayoweza kuboresha fikra za watu”.

Sayyid Swafi amesema kuwa inawezekana kufungua uga wa dua na mafundisho kutoka kwa Ahlulbait (a.s) katika ratiba za masomo ya kujenga uwezo wa watu kwenye sekta mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: