Ugeni wa Ataba unatoa pole kwa kifo cha mzazi wa mashahidi watano Twalibu Abduridhwa Shimri.

Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya unatoa pole kwa kufiwa na mzazi wa mashahidi watano, marehemu Twalibu Abduridhwa Shimri katika mkoa wa Baabil.

Sayyid Naafii Mankushi kutoka kitengo cha mahusiano amesema: “Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya unatoa rambirambi kutoka kwa muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na watumishi wote wa Ataba tukufu, kwa familia ya marehemu na wapenzi wake, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu amuweke mahala pema peponi”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imetoa zawadi ya bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa familia ya marehemu”.

Akaendelea kusema “Ugeni unawajumbe kutoka kitengo cha Dini, usimamizi wa haram, mahusiano, kulinda nidhamu, utumishi na idara ya masayyid”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: