Majmaa-Ilmi inafanya mradi maalum wa kulea vipaji vya usomaji.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inafanya mradi maalum wa kulea vipaji vya usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi (27).

Kiongozi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya Sayyid Haamid Mar’abi amesema, wanafunzi tumewagawa sehemu nne maarufu kwenye mahadhi ya usomaji wa Qur’ani katika ulimwengu wa kiislamu, nazo ni mahadhi ya Haafidh Khaliil Ismail, mahadhi ya kiiraq, Shekhe Minshawi, Shekhe Abdul-Basit Abdul-Swamadu na Shekhe Abu Ainain kwa mahadhi ya kimisri.

Akaongeza kuwa “Mradi unahusisha masomo ya hukumu za tajwidi, sauti na naghma, sambamba na hayo wanafundishwa pia masomo ya Aqida, Fiqhi na Akhlaq.

Akasema kuwa kuwa mradi huu unalenga kulea vipaji vya usomaji wa Qur’ani katika wilaya ya Hindiyya vilivyo gunduliwa wakati wa semina za majira ya kiangazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: