Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amemuonyesha Waziri wa malezi miradi ya Ataba ya kimalezi.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, amemuonyesha Waziri wa malezi Sayyid Ibrahim Naamis Aljaburi miradi ya kimalezi na kielimu inayofanywa na Ataba.

Kikao hicho kimehudhuriwa na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami.

Muheshimiwa katibu mkuu ameeleza miradi ya kielimu na kimalezi inayofanywa na Atabutu Abbasiyya tukufu, na mchango wake katika maendeleo ya taifa la Iraq, na namna shule zao zinavyopata ufaulu mkubwa katika mitihani ya wizara.

Muheshimiwa Waziri amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Atabatu Abbasiyya katika sekta ya elimu na malezi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: