Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan (a.s).
Majlisi imesimamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Ataba tukufu.
Mhadhiri wa Majlisi Shekhe Rashadi Answari amesema “Majlisi itadumu kwa muda wa siku tatu baada ya swala ya Magharibi kwa kuhudhuriwa na mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ambao wanaomboleza kifo cha mjukuu wa Mtume Imamu Hassan Almujtaba (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Muhadhara umeeleza mambo tofauti kuhusu historia ya Imamu Hassan (a.s) na jinsi alivyo jitolea kwa ajili ya Dini sambamba na ukarimu na zuhudi yake, bila kusahau dhulma alizofanyiwa (a.s).
Akaendelea kusema “Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi na qaswida zinazotaja msiba wa Ahlulbait (a.s), zilizo amsha hisia za majonzi na huzuni kwa wahudhuriaji”.
Ataba inaendelea na harakati zake ndani na nje ya mji wa Karbala, inaandaa ratiba ya uombolezaji na kutoa huduma tofauti kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu za Ahlulbait (a.s).













