Majmaa-Ilmi imekamilisha maandalizi ya kufungua kituo cha kutambulisha msahafu mtukufu.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha maandalizi ya kufungua kituo cha kutambulisha msahafu wa Ataba tukufu.

Mkuu wa kituo cha uchapishaji wa msahafu Shekhe Dhiyaau-Dini Zubaidi amesema “Watumishi wetu wamekamilisha maandalizi ya kutambulisha msahafu mtukufu uliochapishwa na Atabatu Abbasiyya miaka tisa iliyopita katika mji wa Karbala, nao ni miongoni mwa mafanikio makubwa ya kituo cha uchapishaji wa Qur’ani tukufu”.

Akaongeza kuwa “Kituo cha kwanza kipo katika maukibu ya Ummul-Banina (a.s) kwenye chuo kikuu cha Al-Ameed Barabara ya Najafu – Karbala na kituo cha pili katika majengo ya Shekhe Kuleini Barabara ya Baghdad – Karbala”.

Katika vituo hivyo anashiriki muandishi wa kituo Sayyid Karaar Mussawi na waandishi wawili mashuhuri, aidha mazuwaru wanapewa nafasi ya kuandika msahafu mtukufu, huku kituo kikiandika majina yao kwenye ukurasa maalum wa watu walioshiriki kwenye tukio hili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: