Kubadilisha bendera ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kumaliza msimu wa huzuni.

Bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imebadilishwa, imetolewa yenye rangi nyeusi na kuwekwa yenye rangi nyekundu, kufuatia kuingia mwezi wa Rabiul-Awwal (1445h).

Kazi ya kubadili bendera imefanywa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Aali Dhiyaau-Dini.

Watumishi wa Ataba wameondoa bendera na mabango meusi kwenye mimbari na korido za haram.

Ubadilishaji wa mapambo meusi umefanyika kufuatia tangazo la ofiri ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani kuwa Jumapili ya kesho ni siku ya kwanza ya mwezi wa Rabiul-Awwal (1445h).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: