Mradi wa Ajru-Risaalah unaofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, unalenga kueleza utukufu wa Ahlulbait (a.s) katika jamii na kujenga maadili mema kwa ujumla.
Mradi unaratiba nyingi za kujenga uwelewa katika mitandao ya kijamii, kwa lengo la kufikia watu wa tabaka tofauti, huandika hadithi zinazohusu Ahlulbait (a.s) hekima na utukufu wao.
Aidha mradi unalenga vijana wenye umri wa miaka 15 – 35, kwani kundi hilo linachangamoto nyingi, pia watu wenye umri huo wanapatikana kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii, hivyo huandika turathi za Ahlulbait (a.s) maswala ya kitamaduni, fiqhi, Qur’ani na mengineyo.
Kuangalia mitandao ya mradi tumia link zifuatazo:
Face book: https://www.facebook.com/ajralrisala1/
Instagram: https://www.instagram.com/ajr_alrisala
Telegram: https://t.me/ajiralrisala
Tiktok: https://www.tiktok.com/@ajr.alrisala?