Wasomaji wa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wameshiriki kwenye hafla ya (kiongozi wa wasomaji wa kitaifa) katika mji wa Karbala.
Hafla imesimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Kiongozi wa idara ya wasomaji katika Maahadi Sayyid Ahmadi Zaamili amesema “Ugeni wa Maahadi ulioshiriki kwenye hafla hiyo umehusisha wasomaji na mahafidhu Zaidi ya (100) ambao ni miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu na wanafunzi wa semina za Qur’ani ambazo hufanywa na idara ya usomaji katika Maahadi.
Akaongeza kuwa “Maahadi kupitia ushiriki wake kwenye vikao vya usomaji wa Qur’ani, inajitahidi kuwajenga wanafunzi kiroho na kuongeza uwezo wao.
Akabainisha kuwa “Waliosoma kwenye hafla hiyo ni Ali Muhammad Zubaidi na Muhammad Ridha Ibrahim.