Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kutoa mihadhara kuhusu Maisha ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na kutoa wito wa kushiriki.
Muhadhara utafanywa chini ya anuani isemayo (Mafundisho ya kujijenga kutoka kwenye Maisha ya Zaharaa (a.s)), na kauli mbiu isemayo (Zaharaa ni utulivu).
Muhadhara utajikita katika kueleza Maisha ya bibi Zaharaa (a.s) kwa lengo la kuchukua mafunzo kutoka kwake.
Muhadhara utatolewa siku ya Jumatano tarehe (6/12/2023m) saa nne asubuhi katika ofisi za kituo mtaa wa Mulhaqu/ Barabara ya Hospitali ya Imamu Hussein (a.s) kwenye jengo la kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s).
Kituo kimetoa wito wa kushiriki kwenye kura za shindandano zitakazo pigwa pembezoni ya muhadhara huo na washindi watapewa zawadi nono.