Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, umefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu.
Kiongozi wa idara ya kupokea wageni katika ukumbi wa utawala ndani ya Ataba tukufu Sayyid Farisi Husseini amesema “Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, ambayo imedumu kwa siku tatu”.
Akaongeza kuwa “Majlisi imepambwa na muhadhara wa kidini uliojikita katika kueleza utukufu wa Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na dhulma aliyofanyiwa (a.s), imehudhuriwa na watumishi wengi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Mhadhiri wa Majlisi Sayyid Ali Rahim amesema “Majlisi imeangazia utukufu wa Bibi Zaharaa (a.s) ambae Mwenyezi Mungu hukasirika kwa kukasirika kwake”.
Akaongeza kuwa “Tumeongea dhulma alizofanyiwa bibi Zaharaa (a.s) ambazo kwa hakika zinapotajwa mwili husisimka, nyoyo hukosa amani na macho hutokwa machozi”.