Wizara ya uadilifu imesema: Makaburi ya Raudhat Jannatul-Kafeel ni sehemu inayo onyesha muongo mbaya katika historia ya Iraq.

Kiongozi mkuu wa idara ya mahusiano katika wizara ya uadilifu Sayyid Ahmadi Laibi amesema, makaburi ya Raudhat Jannatul-Kafeel yanaonyesha muongo mbaya katika historia ya Iraq.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa makaburi ya mfano uliofanywa na Atabatu Abbasiyya katika mji wa Najafu, ambayo wamezikwa watu waliouwawa katika gereza la Badushi.

Akasema kuwa “Ufunguzi wa makaburi ya Raudhat Jannatul-Kafeel ambayo wamezikwa watu waliouwawa kwenye gereza la Badushi katika mji wa Mosul na kundi la magaidi la Daesh, ni kielelezo cha kazi kubwa inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa “Jambo hili linadumisha historia ya maovu ya kundi la kigaidi la Daesh lilipoingia katika miji yetu, na namna lilivyo jaribu kuwagawa raia wa Iraq, kuanzia mauwaji wa wafungwa wa gereza la Badushi ambapo watu (670) waliuwawa kinyama na wengine kuzikwa wakiwa hai kwenye makaburi ya pamoja”.

Akaendelea kusema “Hakika Atabatu Abbasiyya imefanya kazi kubwa ya kuthibitisha jinai za kundi la Daesh, ambazo zilikuwa ni muendelezo wa jinai za chama cha Ba’ath”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: