Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umeshuhudia tukio la kiibada lililofanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Atabatu Abbasiyya hufanya tukio la kiibada kila siku ya Jumanne na Alkhamisi kila wiki, wameanza kwa kusoma ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na wimbo wa (Lahnul-Ibaa) wakiwa wamesimama kwa mistari mbele ya kaburi takatifu, kisha wakaendelea kusoma qaswida zingine.
Tukio hilo limehudhuriwa na mazuwaru wengi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Pamoja na tukio hilo wamekumbuka kifo cha Ummul-Banina (a.s) kwa kuimba qaswida zilizotaja msiba huo mkubwa.
Atabatu Abbasiyya tukufu huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa kuandaa ratiba yenye vipengele tofauti.