Majmaa-Ilmi imekuwa mwenyezi wa kongamano la sita la siku ya kimataifa ya Qur’ani tukufu.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, uongozi wa Wakfu-Shina na baadhi ya taasisi za Qur’ani zimeandaa siku ya kimataifa ya Qur’ani tukufu.

Makamo rais wa Majmaa Dokta Liwaau Atwiyya amesema “Atabatu Abbasiyya hutoa msaada kwa taasisi za serikali na za Qur’ani, leo imekuwa mwenyeji wa viongozi wa taasisi za Qur’ani kutoka Ataba zingine, mazaru, Hashdu-Shaabi na wadao wa Qur’ani kwa ajili ya kuratibu siku ya kimataifa ya Qur’ani tukufu”.

Akaongeza kuwa “Imependekezwa siku ya kimataifa ya Qur’ani tukufu iwe mwezi 27 Rajabu, pia imependekezwa kauli mbiu ya siku hiyo sambamba na baadhi ya mambo yatakayofanywa siku hiyo”.

Akafafanua kuwa “Jambo hili limetokana na wito wa uongozi wa Wakfu-Shia, kupitia kituo cha maarifa ya Qur’ani kitaifa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: