Wajumbe wa Ataba wameeleza kwa ufupi yaliyojiri nchini India na wamekabidhi zawadi na tuzo walizopewa kwaniaba ya Ataba tukufu.
Kikao cha kukabidhi zawadi kimehudhuriwa na wajumbe wa kamati kuu, Sayyid Liith Mussawi, Sayyid Jawadi Hasanawi na rais wa kitengo cha Habari na utamaduni Sayyid Aqiil Yaasiri.
Katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Aalu Dhiyaau-Dini amesema “Leo tumetoa pongezi rasmi kwa wajumbe wa Ataba kutokana na kazi kubwa waliyofanya ya kuratibu kongamano la kiongozi wa waumini (a.s) kwenye maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Ali (a.s), katika msikiti wa Muwakil jijini Mombai katika nchi ya India”.
Akaongeza kuwa “Kongamano hilo limehudhuriwa na Ataba zingine za Iraq, (Atabatu Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya pamoja na waandalizi Atabatu Abbasiyya) lengo la kongamano ni kutoa picha halisi ya kazi zinazofanywa na Ataba tukufu ya kufikisha ujumbe wa Ahlulbait (a.s) ndani na nje ya Iraq”.
Kongamano lilikuwa na harakati tofauti, kupandisha bendera za Ataba tukufu, ufunguzi wa maonyesho ya vitabu, kutembelea hauza na shule za kidini, utowaji wa zawadi, kufanya kikao cha usomaji wa Qur’ani, kupiga kura za bahati nasibu ya Kwenda kufanya ziara katika Ataba za Iraq.