Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imepambwa kwa mauwa kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa wajumuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Idara inayosimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeweka maua kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa kwa wajukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Kiongozi wa idara Sayyid Aqiil Twaif amesema “Watumishi wa idara wameweka mauwa kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) hususan kumbukumbu ya kuzaliwa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Miongoni mwa vipengele vya kuhuisha mazazi ya wajukuu wa Mtume (a.s) ni kupamba juu ya dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa maua mazuri”.

Kawaida Atabatu Abbasiyya huweka maua mazuri ya rangi tofauti na harufu nzuri juu ya dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kuadhimisha mazazi ya Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: