Atabatu Abbasiyya imefanya kongamano la kuzaliwa kwa nuru za Muhammadiyya katika mji wa Hamza mashariki mkoani Qadisiyya.
Kongamano hilo limesimamiwa na kitengo cha mahusiano kupitia idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule kwa kushirikiana na umoja wa wanafunzi wa mji wa Hamza mashariki, ikiwa ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel.
Kiongozi wa idara ya harakati za chuo katika kitengo hicho Sayyid Ahmadi Yasiri amesema “Kongamano linavipengele vingi, ikiwemo ujumbe wa Ataba tukufu uliowasilishwa na Sayyid Adnani Jaluhkani, ujumbe wa umoja wa wanafunzi wa mji wa Hamza mashariki uliowasilishwa na Sayyid Ali Tamimi, muhadhara elekezi uliowasilishwa na Sayyid Jasaam Saidi, yakafuata mashairi na tenzi mbalimbali”.
Akaongeza kuwa “Kongamano likahitimishwa na shukrani kutoka kwa umoja wa wanafunzi, wameishukuru Ataba tukufu kwa kuwajali”.
Kongamano linalenga kuimarisha uwelewa wa kidini na kitamaduni, kujenga misingi ya kuishi kwa amani na upendo, kuimarisha nafasi ya vijana katika jamii na kuwahimiza kushiriki katika harakati za kitamaduni.