Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza majina ya washindi wa shindano maalum kuhusu maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f).
Sharti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Mahadi (a.s) itakayofanywa katika uwanja wa mlango wa Qibla mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Ijumaa (23/02/2024m) sawa na tarehe (12 Shabani 1445h) saa moja na nusu jioni.
Iwapo mshindi atakuwa na udhuru wa kushindwa kuhudhuria, atatakiwa afike kwenye ofisi za wahasibu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya siku nne toka kutanganzwa kwa majina ya washindi, akiwa na kitambulisho cha uraia au hati ya kusafiria.