Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimekamilisha maandalizi ya kuwapokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya mwezi kumi na tano Shabani.
Makamo rais wa kitengo Mhandisi Muhammad Twawiil amesema “Watumishi wa kitengo wamekamilisha maandlizi ya kupokea mazuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani kupitia mkakati maalum wa utoaji wa huduma na ulinzi, sambamba na kuratibu mpangilio wa matembezi ya mazuwaru”.
Akaongeza kuwa “Tumeandaa utaratibu maalum wa utoaji wa huduma na ulinzi kuanzia kwenye vizuwizi hadi katika haram na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili pamoja na kuchukua tahadhari zote muhimu” akasema “Kitengo Kitagawa maji, chakula na mengineyo kwa mazuwaru wa malalo mbili takatifu”.
Akaendelea kusema “Watumishi wetu watatumia uwezo wao wote katika kudumisha usafi kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu”