Kitengo cha usafiri katika Atabatu Abbasiyya kimejiandaa kupokea mazuwaru wanaokuja kuadhimisha mazazi ya Imamu Mahadi (a.f).
Rais wa kitengo muheshimiwa Alaa Ammaar Yaasir amesema “Watumishi wetu wanafanya kila wawezalo katika kuhudumia mazuwaru wanaokuja kuhuisha maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f) katika usiku wa mwezi kumi na tano Shabani”.
Akaongeza kuwa “Kitengo kimeandaa gari nyingi kwa ajili ya kubeba mazuwaru watukufu”.
Akaendelea kusema “Mkakati wa pili ni utoaji wa huduma, kitengo kimeandaa gari za utoaji wa huduma za vyoo vya dharura, gari za kusambaza maji, gari za utoaji wa huduma za afya sambamba na kuandaa gari kwa ajili ya vitengo vingine kulingana na mahitaji yao”.