Kiongozi wa idara ya harakati katika Majmaa-Ilmi Sayyid Wahaaji Abaadi amesema “Mashindano yamehusisha vikundi (14) vya vijana wenye umri wa chini ya miaka ishirini, nayo ni miongoni mwa mashindano muhimu, yanaongozwa na majaji wenye kiwango cha juu kutoka Ataba na wanafunzi wa hauza”, akabainisha kuwa “Kazi ya kuchagua washiriki wa mashindano haya ilifanywa kwa kupitia upigaji wa kura”.
Akaongeza kuwa “Kupitia mashindano haya, kituo kinatumia vizuri mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii sambamba na kufanyia kazi ndoto ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.