Makundi ya mazuwaru yamehuisha usiku wa Lailatul-Qadri wa pili, na kuomboleza kifo cha Imamu Ali Bun Abu Twalib (a.s) kwa kunyanyua misahafu mbele ya malalo yake takatifu katika mji wa Najafu.
Mji wa Najafu umeshuhudia makundi makubwa ya waombolezaji, yamekuja kufanya ziara na kusoma dua za usiku wa (21) katika mwezi wa Ramadhani (Lailatul-Qadri ya pili), na kuomboleza kifo cha Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).
Mazuwaru huhuisha usiku huu kwa kusoma dua maalum, kuinua misahafu, kusoma Qur’ani na kufanya (vikao) Majlisi za kuomboleza.