Wahudumu wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya wameomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s) kwa kufanya maukibu ya pamoja.
Maukibu imeanza matembezi yake kutokea ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kusimama kwa mistari na kuelekea katika malalo ya Imamu Hussein (a.s), wakipitia uwanja wa kataikati ya harama mbili huku wanaimba qaswida za kuomboleza zinazotaja msiba huo mkubwa kwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s).
Maukibu ikahitimisha matembezi yake katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) kwa kufanya majlisi ya kuomboleza, iliyohudhuriwa na watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na kundi kubwa la mazuwaru, Majlisi ikapambwa na qaswida na tenzi za kuomboleza.
Wahudumu wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala, hufanya maukibu ya kuomboleza kwenye kumbukumbu ya vifo vya Ahlulbait (a.s).








































