Atabatu Abbasiyya imemkaribisha rais wa Wakfu-Shia na muwakilishi wa Ataba tukufu.

Atabatu Abbasiyya imemkaribisha rais wa Wakfu-Shia Dokta Haidari Shimri, katibu mkuu wa Atabatu Askariyya na muwakilishi wa Ataba tukufu.

Ugeni huo umekutana na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi mbele ya katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu.

Rais wa Wakfu-Shia Dokta Haidari Shimri amesema “Tumepata heshima katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ya kukutana na viongozi wa Ataba tukufu wanoratibu na kuendesha shughuli za kuhudumia malalo takatifu na mazuwaru wake watukufu”.

Akaongeza kuwa “Katika kikao hicho tumejadili namna ya kuongeza juhudi na kusaidiana baina ya Ataba, kwa ajili ya kufikia malengo ya kuhudumia mazuwaru na kufundisha mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.

Ugeni umefanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa Wakfu-Shia ameonyesha furaha kubwa kwa kufanya ziara hiyo, amepongeza kazi nzuri zinazofanywa na wahudumu wa malalo na amewatakia mafanikio mema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: