Ukanda wa kijani kibichi unajiandaa kupokea familia za watu wa Karbala katika siku za Idul-Fitri

Ukanda wa kijani kibichi unajiandaa kupokea familia za watu wa Karbala na mazuwaru katika siku za Idul-Fitri.

Mradi wa ukanda wa kijani uliopo kusini mwa mji wa Karbala, umepokea mamia ya familia za watu wa Karbala toka kuanza kwa mwezi wa Ramadhani, wahudumu wa mradi huo wameandaa kila kinachohitajika katika kupokea wageni wanaokuja katika ukanda wa kijani kwenye siku za Idul-Fitri.

Mradi unajumla ya viwanja (24) ambavyo hupokea watu, vinasehemu za kupumzika, vyoo na mazingira safi na tulivu.

Atabatu Abbasiyya inaendelea kufanya upanuzi wa sehemu ya ukanda wa kijani, kwa lengo la kuhudumia watu wengi zaidi na kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya kupambana na uharibifu wa mazingira unaoshuhudiwa nchini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: