Wahudumu wa Ataba mbili tukufu wameomboleza kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii.

Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wameomboleza tukio la kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s) kupitia maukibu ya uombolezaji.

Mshauri wa katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Faadhil Auz amesema “Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kila mwaka hufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani na majlisi za kuomboleza tukio la kuvunjwa makaburi ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) katika eneo la Baqii-Gharqad”.

Akaongeza kuwa, miongoni mwa harakati ambazo hufanywa kila mwaka kwenye maombolezo hayo, ni maukibu ya pamoja baina ya wahudumu wa malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ushiriki wa mazuwaru ambapo hutoa pole kwa bwana wa mashahidi (a.s) kufuatia tukio hilo la kuhuzunisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: