Kitengo cha habari na utamaduni kimejadili njia za kushirikiana na taasisi ya muongozo wa masomo na utafiti.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimejadili njia za kushirikiana kielimu na kitamaduni na taasisi ya muongozo wa masomo na utafiti chini ya Atabatu Husseiniyya.

Kikao kimehusisha kituo cha tafiti za kiislamu na kimkakati chini ya kitengo na taasisi ya muongozo wa usomaji na utafiti chini ya Atabatu Husseiniyya, wamejadili vipengele vya kielimu vinavyo waonganisha.

Wamejadili kuhusu kuanzishwa harakati ya pamoja, kufungua maktaba ya kwenye mtandao, kuweka mikakati ya miradi ya kielimu yenye malengo ya Dini.

Kikao hiki ni sehemu ya kuonyesha ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya, kwa lengo la kuitumikia elimu chini ya mwenendo wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: