Kamati ya maandalizi ya wiki ya Imamu kielimu na kimataifa awamu ya pili, imetangaza msimamo wa nusu mwezi kuhusu mada za kongamano kuhusu Imamu Sajjaad (a.s).
Kongamano la Imamu Sajjaad (a.s) ni sehemu ya shughuli za awamu ya pili ya wiki ya Imamu kielimu na kimataifa chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyo tengana), mada zitajikita katika kueleza (Mwenendo wa Maimamu katika kulea mtu na umma).
Kongamano litasimamiwa na kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tarehe (30/6/2024m) sawa na (23 Dhulhijjah 1445h).
Kitengo kimepokea mihtasari ya mada (22) na tafiti za kielimu (29) kutoka nchi tofauti za kiarabu na kiislamu.
Mada zinafafanua athari za riwaya za Imamu Sajjaad (a.s) katika elimu ya Qur’ani, tafsiri, maadili ya kidini, Aqida, Fiqhi, malezi ya nafsi (saikolojia), jamii, utamaduni na afya.