Majmaa-Ilimi katika Atabatu Abbasiyya kupitia Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu inatoa mihadhara ya kuwajengea uwezo walimu wa Qur’ani katika majira ya kiangazi kwenye mkoa wa Diwaniyya.
Semina inahusisha kujadili njia za ufundishaji na nafasi ya mwalimu katika kitengeneza kizazi chema kinachofata mwenendo wa vizito viwili na kuboresha uwezo wa walimu.
Jumla ya walimu (110) kutoka wilaya na mitaa tofauti itakayokuwa na semina kuanzia tarehe ishirini mwezi huu wa nne wameshiriki kwenye semina hiyo, semina zitakazo fanywa zinatarajiwa kuchukua wanafunzi (5250).
Maahadi inafanya semina za kuwajengea uwezo walimu katika mikoa ya (Misaan, Waasit, Diwaniyya, Najafu, Kirkuuk na Swalahu-Dini) semina zitakazofanywa majira ya kiangazi zinatarajiwa kupata wanafunzi zaidi wa (30000).