Atabatu Abbasiyya imeweka muonekano wa furaha katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Ridhwa (a.s).

Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya, wameweka mazingira ya furaha katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Ridhwa (a.s).

Makamo rais wa kitengo Shekhe Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Watumishi wa kitengo wameweka mabango yanayo ashiria furaha na sifa za Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) katika maeneo ya Ataba tukufu, kwa ajili ya kuadhimisha mazazi yake matukufu”.

Akaongeza kuwa “Kazi ya kuweka mabango imehusisha kuta na milango ya Ataba tukufu, sambamba na kupamba Barabara zinazo elekea kwenye haram tukufu, aidha tumeandaa mazingira ya kufanya hafla kubwa katika uwanja wa mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na hafla zingine za nje zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya katika maeneo tofauti”.

Watumishi wa kitengo hiki kwenye kila kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Maasum (a.s) hugawa marashi na mauwa kwa mazuwaru wanaokuja katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: