Kituo cha utamaduni wa familia kimeanza kusajili washiriki wa semina ya namna ya kuamiliana na hasira.

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kimeanza kusajili washiriki wa semina ya (mikakati ya kuamiliana na hasira) sehemu ya pili.

Semina itakuwa na mada tofauti, miongoni mwa mada hizo ni, namna ya kutambua sababu za kukasirika na jinsi ya kupambana nazo, namna ya kujizuwia katika mazingira magumu, mikakati ya kuamiliana na hasira na kuzifanya kuwa Chanya.

Semina itafanywa siku ya Jumamosi tarehe 25 – 5 – 2024m, saa 4:00 asubuhi.

Mwisho wa semina kutakuwa na mtihani na watakaojibu vizuri watapewa zawadi baada ya kupiga kura kwa washiriki.

Kwa yeyote anaependa kujisajili ajiunge na link ifuatayo: https://t.me/alecture1
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: