Waziri wa mambo ya Ndani Muheshimiwa Abdul-Ameer Shimri alipotembelea mpaka wa Ar’uri, amesifu Atabatu Abbasiyya kwa kuimarisha ulinzi wa misafara ya mahujaji na kuwapa huduma mbalimbali.
Muheshimiwa amesema: “Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanashiriki kuimarisha ulinzi katika misafara ya mahujaji kwenye mpaka wa Ar’uri sambamba na jeshi la Serekali”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imeweka watumishi wake barabara nzima, wanaotoa huduma mbalimbali kwa mahujaji, miongoni mwa huduma huzo ni afya na chakula”.
Blugedia wa kikosi cha Abbasi (a.s) Saadi Maliki Hashim amesema “Kikosi kinasaidia kuweka ulinzi kwenye misafara ya mahujaji kwa kushirikiana na viongozi wa jeshi la serikali wa mkoa wa Karbala”.
Atabatu Abbasiyya imeandaa zaidi ya watumishi wake (1000) kuja kutoa huduma mbalimbali kwa mahujaji na kuimarisha ulinzi wa misafara yao, imekuwa ikifanya hivyo toka mwaka 2015m.