Kuhitimisha kwa ratiba ya kila wiki ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya.

Kamati inayosimamia program maalum ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya imemaliza ratiba ya wiki ya pili katika mwezi wa tatu wa program hiyo kwa watumishi wa Ataba tukufu.

Program hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuwajengea uwezo watumishi wa Ataba, inaendeshwa kwa kushirikiana na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, inahusisha utoaji wa mihadhara mbalimbali, mashindano, safari za kitalii na kidini.

Ratiba hudumu siku tano kwa kila kikundi cha watumishi wa Ataba, ambapo hufundishwa mambo yanayo wajenga kiimani na kuimarisha maelewano baina yao, sambamba na kuwaonyesha shughuli zinazofanywa na Ataba tukufu katika sekta ya elimu, malezi, utoaji wa huduma, kilimo na viwanda.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: