Majmaa-Ilmi imesema: Karibu wanafunzi (4000) wanashiriki kwenye mradi wa semina za Qur’ani katika mkoa wa Karbala.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imesema kuwa, idadi ya washiriki wa mradi wa semina za Qur’ani katika mji wa Karbala imekaribia wanafunzi (4000).

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Karbala Shekhe Jawadi Nasrawi amesema “Mwaka huu mradi wa Qur’ani umepokea zaidi ya wanafunzi (3800) katika mji wa Karbala na maeneo ya Jirani”.

Akaongeza kuwa “Vikao vya washiriki wa mradi huo vinafanywa ndani ya Haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), majengo ya makazi ya Abbasi, misikiti na husseiniyya zilizopo katika mji wa Karbala na pembezoni mwake”.

Akafafanua kuwa “Wanafunzi wanapata masomo yao kutoka kwa walimu (150), wengi wao ni wahitimu wa Maahadi katika masomo ya ubobezi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: