Kituo cha kuhuisha turathi chini ya kamati kuu ya kuhuisha turathi katika Atabatu Abbasiyya kimechapisha kitabu cha (Rasaailu-Fiqihiyya) kilicho andikwa na Sayyid Hussein bun Muhammad Ibrahim Qazwini (kf: 1208h).
Makamo mkuu wa kituo Shekhe Dhiyaau Karbalai amesema “Turathi za Sayyid Qazwini zipo nyingi na aina tofauti, zinashuhuda Madhubuti, mada makini, ameandika Rasaailu-Fiqihiyya katika Ibadaat na Muamalaat, ambayo ni saya Risala arubaini, tumechapisha tano katika awamu ya kwanza”.
Akaongeza kuwa “Tutaendelea kuchapisha zilizobaki, baadhi tumezifanyia uhakiki na zingine bado tunaendelea kuzikusanya na kuzihakiki”.
Akabainisha kuwa “Awamu ya kwanza inarisala zifuatazo (Sherehe ya risala ya khiyari katika uuzaji ya muhakiki Karki, hukumu ya kuuza wakfu, kufanya ibada katika eneo lisilohalali, haki ya kuelewana na adui wako inaposhindikana kutoa hoja, hukumu ya Wanyama na wadudu kuhusu uhalali wa kuliwa kwao”.