Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imehudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru waliojaa huzuni kutokana na msiba huo mkubwa kwa wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s).
Majlisi yatadumu kwa muda wa siku tatu ambapo itakuwa ikifanywa asubuhi na jioni.
Mhadhiri wa leo Sayyid Majidi Mubarqaa ameongea kuhusu Maisha ya Imamu Aljawaad (a.s) na njama alizofanyiwa na utawala wa Bani-Abbasi.
Akahimiza kufuata mwenendo wa Imamu (a.s), kwa kuvumilia na kubeba majukumu ya kutumikia Dini na binaadamu kwa ujumla.
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi na mashairi yanayomuhusu Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).
Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum yenye vipengele tofauti kwa ajili ya kuomboleza msiba huo.