Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa, Shekhe Jawadi Nasrawi amesema “Maahadi imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) mbele ya wanafunzi wa mradi wa Qur’ani katika majira ya kiangazi”.
Akaongeza kuwa “Lengo la kufanya Majlisi ni kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s), matukio ya mazazi au vifo, sambamba na kuangazia mafundisho yanayopatikana katika Maisha yao matukufu”.
Akabainisha kuwa “Mradi wa semina za majira ya kiangazi unalenga utamaduni wa kufanyia kazi vizito viwili Qur’ani na kizazi kitakasifu (a.s)”.