Waziri wa umeme Mhandisi Ziyadi Ali Faadhil, amepongeza mchango wa Atabatu Abbasiyya katika umeme kwenye mkoa wa Karbala.
Ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea na kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Muheshimiwa amekutana na mshauri wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Twalaal Biir, na kusikiliza maelezo kuhusu baadhi ya miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya kwa mazuwaru na jamii.
Waziri wa umeme amepongeza mchango mkubwa unaotolewa na Ataba katika kusaidia upatikanaji wa umeme, akasema kuwa mchango huo umepunguza kwa kiwango kikubwa matatizo ya umeme katika mkoa wa Karbala.
Akaongeza kuwa “Ziara yetu katika Atabatu Abbasiyya inalenga kuangalia maandalizi ya pamoja baina yetu na Ataba tukufu katika mwezi wa Muharam na ziara ya Arubaini”.