Miongoni mwa mfululizo wa hafla za mimbari za nuru.. Majmaa-Ilmi imefanya hafla ya kuadhimisha Idul-Ghadiir.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya kuadhimisha sikukuu ya Idul-Ghadiir, ikiwa ni sehemu ya hafla za (mimbari za nuru).

Hafla hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Ghadiir yanayofanywa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa-Ilmi na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wanafunzi wa mradi wa (kiongozi wa wasomaji) na walimu wao.

Hafla ilikuwa na vipengele tofauti, usomaji wa Qur’ani kwa sauti ya msomaji wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Ammaari Alhilly, qaswida kutoka kikosi cha Mazamiru-Thaqalaini kutoka Misaan na qaswida za kimashairi kuhusu Imamu Ali (a.s) kutoka kwa Mula Maahir Sultani Karbalai.

Washiriki wamepewa zawadi za kutabaruku kutokana na Baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: