Ataba inafanya kongamano la wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Mfumo wa Maimamu –a.s- katika kulea mtu na umma) kuanzia tarehe 27/6/2024m hadi 4/7/2024m.
Mkuu wa kituo cha miradi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Hasanaini Halo amesema “Majmaa-Ilmi imeandaa kikao cha usomaji wa Qur’ani ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa washiriki wa wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili”.
Akaongeza kuwa “Kikao kimeshuhudia wasomaji tofauti wa Qur’ani kutoka ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya na usomaji wa pamoja kutoka kwa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji kitaifa”.
Kikao cha usomaji wa Qur’ani ni sehemu ya maelekezo ya Atabatu Abbasiyya, yanayolenga kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani tukufu.
Atabatu Abbasiyya inafanya kila iwezalo katika kuonyesha elimu ya Ahlulbait (a.s) na historia yao katika kutatua changamoto sambamba na kubainisha nafasi yao (a.s) katika kupambana na fikra potofu.