Sayyid Swafi amepokea kundi la walimu wa Hauza ya Qum takatifu.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amepokea kundi la walimu wa Hauza ya mji mtukufu wa Qum.

Amekutana nao pembezoni mwa kongamano la wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili inayosimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, amewakaribisha na kuwapa pongezi za sikukuu tukufu ya Ghadiir.

Ugeni umehusisha Shekhe Ali Maruji Qazwini mwalimu mkubwa wa Bahthu-Khariji na walimu wengine wa ngazi hiyo, Sayyid Ahmadi Twabatwabai Turbati, Shekhe Hussein Shabii, Sayyid Baaqir Mussawi Asfahani mwalimu wa Sutuuhu ya juu na mhakiki Shekhe Muhammad Issa Albanai.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya wiki ya Imamu na mshauri wa kamati kuu ya kuhuisha turathi za Atabatu Abbasiyya Shekhe Muslim Radhwai amesema “Ugeni umepongeza kazi nzuri inayofanywa na Atabatu Abbasiyya kwa kufanya makongamano ya kielimu na kitamaduni, likiwemo kongamano hili lililoalika hauza tukufu mbalimbali”.

Ugeni umesisitiza umuhimu wa makongamano ya kielimu katika uwanja wa kitamaduni.

Ugeni wa walimu wa hauza kutoka Qum, wamemshukuru Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya kwa namna anavyo saidia wanachuoni na walimu wa hauza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: