Atabatu Abbasiyya tukufu imeshuhudia shughuli ya wahitimu wa chuo cha askari awamu ya nne.
Mamia ya wanafunzi wa kikosi cha (87) wamesoma kiapo cha kuhitimu katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya kundi kubwa la wazazi na mazuwaru.
Wahitimu wamefanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kutabaruku katika mgahawa wa Abulfadhil Abbasi.
Mamia ya wahitimu wa vyuo vya Askari na vyuo vikuu vya Iraq husoma kiapo cha kuhitimu kila mwaka ndani ya haram za Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.