Mawakibu za watu wa Karbala zinafanya matembezi ya kuomboleza, zikielekea kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) jioni ya siku ya kwanza katika mwezi wa Muharam.
Kumi la kwanza la mwezi wa Muharam ni maalum kwa mawakibu za watu wa Karbala, ni utamaduni uliozoweleka toka zamani, huanza matembezi za mawakibu za (zanjiil).
Mawakibu nyingi za kuomboleza zimejitokeza leo siku ya Jumatatu, katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, chini ya utaratibu uliozoeleka kila unapoingia mwezi wa Muharam.
Mawakibu hufanya maombolezo kwa kufuata utaratibu maalum unao andaliwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya, hutumia barabara maalum zinazoelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), huingia katika haram yake tukufu kisha hutoka na kuelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) kwa kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Kitengo cha maadhimisho huandaa kikosi maalum cha watumishi wake ambao hufuatana na mawakibu kuanzia mwanzo hadi mwisho, jukumu lao ni kusimamia matembezi na kuzuwia muingiliano wa mawakibu au na mazuwaru.