Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) katika mji wa Kaduna nchini Naijeria.
Majlisi imeandaliwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya na kuhudhuriwa na kundi kubwa la wapenzi wa Ahlulbait (a.s).
Mubalighi wa Markazi katika mji huo Sheikh Ibrahim Mussa Yusufu ametoa muhadhara wenye anuani isemayo “Utukufu wa kumlilia Imamu Hussein (a.s) kutokana na kauli za maasumina –a.s-”, majlisi hiyo ni sehemu ya ratiba ya Markazi katika bara la Afrika.
Markazi Dirasaati inafanya mafundisho ya Dini kupitia majlisi za kuomboleza, aidha imekuwa ikihuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) daiama kwa lengo la kujenga uwelewa wa Dini katika jamii za waafrika