Majmaa-Ilmi inafanya majlisi ya kuomboleza katika mwezi mtukufu wa Muharam

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza katika wilaya ya Hindia mkoani Karbala.

Majlisi imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Hindiyya chini ya Majmaa, kwa ushiriki wa wanafunzi wa mradi wa kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na kukihifadhi.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kutoka kwa Hussein Qazwini, ukafuata muhadhara kutoka kwa Shekhe Muhammad Mahadi Samawi, ameeleza tukio la kuuawa kwa Imamu Hussein, watu wa nyimbani kwake (a.s) na wafuasi wake, akawataka wanafunzi kufuata mwenendo wa Abul-Ahraar (a.s) na kuchukua somo na mazingatio katika Qur’ani tukufu.

Majlisi ikahitimishwa kwa ushiriki wa muimbaji Ahmadi Dhabihawi, amesoma qaswida na tenzi zinazoeleza tukio hilo la kuumiza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: