Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inatoa mihadhara elekezi kwa wanafunzi wa semina za kidini.
Kiongozi wa Maahadi Bibi Manaar Aljaburi amesema “Mihadhara inatolewa kwa kushirikiana na kituo cha utamaduni wa familia chini ya Ataba, kwa lengo la kujenga watu wenye maadili na uwezo wa kupambana na changamoto”.
Akaongeza kuwa “Maahadi kwa kushirikiana na idara ya maelekezo ya kifamilia katika Ataba, ilitoa mihadhara elekezi kwa wanafunzi wa semina za majira ya kiangazi, na hivi sasa inatoa mihadhara ya aina hiyo kwa wanafunzi wa Dini”.
Akabainisha kuwa “Walimu waliobobea katika mambo ya familia wametoa mihadhara iliyojikita katika kueleza mazingira halisi ya wasichana wa shule za msingi, sekondari na chuo kwa lengo la kuwawezesha kupambana na changamoto za kijamii”.